Saturday, February 2, 2013

NAMPENDA SANA MAMA YANGU

Thuwein Thabit,

Namshkuru sana Mungu muumba wa kila kitu kwa kunijaalia kuwepo duniani kupitia kwenye mgongo wa mama yangu. Shukrani pia ziende kwa mama yangu ambae amesimamia makuza yangu tangu udogoni mpaka ukubwani, na kwa kweli kabisa naweza sema mama ni muhimu katika kila nifanyalo.

Fatma Haji Choum ni mama yangu wa damu ambae amenizaa ambapo kwa bahati nzuri mpaka leo yu hai huku nikimuomba Mungu ampe umri mrefu wenye kheri naye. Nimezaliwa tarehe 29, Ogasti, 1991 katika hospitali ya Mwembeladu. Wakati huo mama yangu alikuwa akiishi mtaa mmoja hapa Zanzibar ujulikanwao kama Migombani. Makero mengi sana nimeyafanya kwa mama yangu wakati nilipokuwa mdogo kama ada ya mtoto kwa mama au mlezi wake. Lakini licha ya yote hayo mama yangu alinipa upendo wa dhati na kunienzi kwa vile nilikuwa ni mtoto wa mwanzo wa kiume katika familia yetu.

Bila ya kusahau mama yangu amechangia mafanikio mengi tu mpaka sasa ambayo nimeyapata. Miongoni mwao ni kuwa nimepata elimu bora na kazi nzuri pamoja na maadili mema ayapasayo kuwa nayo mtoto katika jamii yetu ya Watanzania. Kufuatia yote hayo najihisi ni mwenye bahati sana katika maisha.

1 comment:

Unknown said...

Nadhani huu ni wakati wa kulipa fadhila kwa wazazi wanguuuuuu