Wednesday, September 5, 2012

FAHARI YA WANAUME WENGI MJINI

Hivi nikimzungumzia mwanamke na thamani aliyonayo mbele ya mwanaume sidhani kama nitakuwa nimefanya makosa. Kwa maana ya haraka, mwanamke ni sawa na tunda lenye thamani sana mbele ya mwanamme. Mvuto na ucheshi wa mwanamke huwavuta wengi miongoni mwa wanaume.

Watu wengi hudhani kuwa mwanamke ni chombo cha starehe katika jamii. Usemi huo ingawa hauna uhalisia lakini mara nyengine hudhihirika kuwa ni wenye ukweli ndani yake. Ni jambo la kujivunia sana kuwa kwa namna japo chache sana, Tanzania ni nchi ambayo bado imeendelea kudumisha mila na silka za Mwafrika. Mitaani wasichana wengi hushangaza sana mbele ya wanaume shababi, ingawa huwa ni wabishi. Si jambo la kukanusha kuwa Tanzania katika majia ya miji wanaume hupishana na wanawake ambao huvaa mavazi ya aina kwa aina.

Wanaume wengi huwa ni wenye kuvutiwa na wanawake wanaovaa mavazi yasiyo ya kawaida, na hali hiyo huchochea kuongezeka kwa vitendo vya kujamiiana nchini, hali ambayo huababisha ongezeko la maradhi mbali mbali ya zinaa hasa Ukimwi. Umefika wakati Watanzania wote tubadilikeni!

Thuwein Thabit
05, Septemba 2012

No comments: